Magoli mawili ya Robert Lewandowski yaibeba Bayern Munich - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 21, 2017

Magoli mawili ya Robert Lewandowski yaibeba Bayern Munich


Mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani wa Freiburg VS Bayern Munich ambao ulikua mgumu kwa pande zote mbili.

Freiburg walijipatia goli lakuongoza katika dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa Janik Haberer. Munich walikuja kusawazisha goli dakika ya 35 kupitia kwa Lewandowski. Goli la pili na goli la ushindi la Munich limepatikana katika dakika za nyongeza za mchezo ambapo dakika ya 91, Lewandowski akarudi kwa mara nyingine tena.

Bayern Munich inaongoza ligi kwa jumla ya alama 42 kwa sasa ikiwa na tofauti ya alama 6 na timu ya RasenBallsport ambao wana mechi moja mkononi.

Post a Comment