Mechi kali tatu: Samatta atisha; Di Maria apiga kamba kali; Napoli yaendeleza ubabe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 25, 2017

Mechi kali tatu: Samatta atisha; Di Maria apiga kamba kali; Napoli yaendeleza ubabeMchezo mmoja umechezwa leo katika mashindano ya Coppa Italia ambapo napoli imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1 - 0 dhidi ya Fiorentina kupitia kwa Callejon katika dakika ya 71. huku mechi ikimaliza kwa kua na kadi mbili nyekundu moya ya Hysaj wa Napoli na ya pili ya Olivera wa Fiorentina.


Bordeaux 1 - 4 Paris Saint-German ni ushindi mnono wa PSG katika kombe la ligi. Mshambuliaji Cavani kafunga mabao mawili na pia Di Maria kafunga mabao mawili na bao lakufutia machozi la Bordeaux limefungwa na Diego RolanTimu ya Genk anayoichezea Mbwana Samatta yaibuka na ushindi wa magoli 3 - 0 dhidi ya timu ya Kortrijk huku mchezaji Mbwana Samatta akiifungia timu ya Genk goli la pili katika dakika ya 42 baada ya kupiga kichwa matata sana. Mungu mbariki Mbwana Samatta, Mungu ibariki Tanzania.

Post a Comment