Mo Farah Kukumbana na Uamuzi wa Donald Trump - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 31, 2017

Mo Farah Kukumbana na Uamuzi wa Donald TrumpHaijalishi uwe na Visa halali au sio halali, muhamiaji halali au sio halali kutoka nchi kama Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, kwa sasa hakuna nafasi ya kuingia nchini Marekani mpaka siku 90 kumalizika.

Uamuzi huo wa Trump umewafanya mashabiki wa mchezo wa riadha kuwa na hofu juu ya Mo Farah ambaye ana uraia wa nchi mbili na moja ya nchi anayotoka imezuiliwa na Trump kwa waislamu kuingia nchini humo, Mo Farah ni mzaliwa wa Somalia ambaye makazi ya mazoezi yake pamoja na familia yake nayo wanaishi nchini Marekani.

Farah anaishi huko Oregon Marekani na inafahamika kwamba laiti kama angelikuwa bado yupo hapo Marekani isingekuwa rahisi kuondolewa lakini sasa Bad Newz ni kwamba nyota huyo hayupo nchini Marekani, inasemekana yupo Ethiopia kimazoezi na jambo hilo litamfanya kutopata nafasi ya kurudi kwa familia yake.
Post a Comment