Mshindi wa Ubunge Dimani aahidi kuwa daraja - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 24, 2017

Mshindi wa Ubunge Dimani aahidi kuwa daraja

Mshindi wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar Juma Ali Juma ameahidi kuzibeba kero za wananchi wa jimbo hilo na kuwasilisha serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa haraka

Ametoa ahadi hiyo mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Fatma Gharib Ali kumtangaza rasmi kuwa mshindi katika uchaguzi huo na kusema kuwa kuwa Ubunge ni daraja la wananchi na serikali

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Hafidh Ali Tahir akiwa Bungeni Dodoma na umehusisha wagombea kutoka vyama 11 vya siasa.

Juma Ali Juma amepata kura 4,860 na kumshinda mpinzani wake kutoka CUF, Abdulrazak Khatib Ramadhan aliyepata kura 1,234.

Katika Uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 6, 172 kati ya wapiga kura 9,275 waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura jimboni humo.

Katibu wa Idara Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar amesema ushindi wa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi huo umekuwa mkubwa kuliko ule wa uchaguzi wa mwaka 2015, ishara inayotoa matumaini ya kuwa wananchi wa jimbo hilo wanaendelea kuiunga mkono CCM.
Post a Comment