Ligi ya Uingereza: Man City yang'ara; Man U yapata sare tasa: Everton yakwama. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 2, 2017

Ligi ya Uingereza: Man City yang'ara; Man U yapata sare tasa: Everton yakwama.


Mchezo kati ya West Harm United dhidi ya Manchester City umemalizika huku timu ya Man City ikiweza kuibuka kwa ushindi wa mabao 0 - 4. Wafungaji Bruyne dakika ya 17, David Silva dakika ya 21, Gabriel Jesus dakika ya 31 na Yaya Toure katika dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati.
Man U imetoka bila bila na Hull City. Man U imeshika namba 6 huku ikiwa na alama 42 huku ikiwa imeongeza kwa kuachwa na alama 4 na Man City ambao wapo nafasi ya 5.

Stoke City 1 - 1 Everton.
Timu ya Everton imekwama kupunguza nafasi ya alama na timu namba 6 ambayo ni Man U baada ya kukubali sare ya bao 1 - 1. Goli la kwanza limefungwa na Peter Croach dakika ya 7 ya mchezo; huku goli la Everton limepatikana baada ya Ryan Shawcross wa timu ya Stoke City kuifunga.
Post a Comment