Mzee Mandela aliniambia nimuoe mwanae - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 9, 2017

Mzee Mandela aliniambia nimuoe mwanae


Boateng aliweza kubadiri uraia wa Ujerumani ambako aliwakilisha katika levo ya ujana na kubadili kua raia wa Ghana. Katika muda huo alikua mtu muhimu katika kikosi cha mpira wamiguu cha nchi ya Ghana.

Timu ya taifa ya Ghana iliweza kukutana na raisi wa zamani wa Afrika ya kusini Nelson Mandela, ambapo kwa upande wa Boateng ilikua moja ya ndoto yake imetimia.

Mchezaji Boateng alipokua akihojiwa na The Guardian alisema "Kuna watu watatu ambao muda wote nilitaka kukutana nao: Micheal Jackson, Muhammad Ali na Nelson Mandela". Lakini nimeweza kukutana na mmoja tu na ni ngumu kuelezea ila imebaki kua furaha".

Mandela alifungwa jela kwa muda wa miaka 27 kwa sababu ya uwelewa wa haki zake ambaye alikua jela na baadae alitoka.

"Mandela alitakiwa kuwa na chuki kwa dunia nzima lakini hali haikua hivyo, kwake ilikua ni shwari na katika kiti chake kidogo alisema hello kwa kila mtu, alifanya unajisikia shwari muda wote. Alikua anang'aa. Ilikua kama filamu. Ilikua kama malaika amekaa pale"

"Tuliingia kwenye chumba chake: Hello... Hello... Alitikisa mkono wangu, alinivuta mbele kwake na akasema: 'Binti yangu anataka umuoe wewe.'

Boateng alijibu 'Nishapata rafiki wa kike teyari, samahani'

Mandela "Hapana, hakuna lakini ninao wengine wazuri zaidi'   baada ya haya maneno kila mmoja alicheka

Tulishindwa kupiga picha kwasababu mwanga wa kamera unamuumiza macho yake lakini ninayo moja tu. Lakini hata hainioneshi sura kama mimi na ni ngumu kuamini'


Post a Comment