Tazama video kwa ufupi jinsi Cameroon ilivyoshinda ubingwa kombe la AFCON 2017 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 6, 2017

Tazama video kwa ufupi jinsi Cameroon ilivyoshinda ubingwa kombe la AFCON 2017
Timu ya taifa ya Cameroon imeibuka na ushindi wa mabao 2 - 1 dhidi ya timu ya taifa ya Misri. Mpira ulikua wakuvutia muda wote. Kutangulia kwa timu ya Misri kupata goli kali la kuongoza kupitia kwa Elneny kulipa hima sana wachezaji wa Cameroon kujituma zaidi na kuziba mapengo yaliojitokeza awali, ila baadae dakika ya 58 Cameroon walipata goli la kusawazisha kupitia kwa N'koulou ambaye alipata nafasi yakupiga kichwa matata sana, huku goli la lala salama limefungwa dakika ya 87 kwa umakini mkubwa wa mchezaji Aboubakar baada ya kuwachanganya mabeki wawili na kumuacha kipa akiduaa baada ya kupata sinto fahamu ya jinsi mpira ulivyopigwa.

Tazama mechi ya fainali hapa kwa ufupi

Post a Comment