Padri afunga ndoa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 28, 2017

Padri afunga ndoa


Miaka tisa baada ya kuvuliwa daraja la upadri wa Kanisa Katoliki, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, Privatus Karugendo amefunga ndoa na Rose Birusya.

Ndoa hiyo ilifungwa jana katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini hapa katika misa iliyoongozwa na Padri Stefano Kaombe.

Mapadri wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa na wanapoachishwa husubiri kibali maalumu kutoka kwa kiongozi wa kanisa hilo duniani.

Akiwa mwenye furaha, Karugendo alizungumza kwa simu na mwandishi wetu kwa dakika chache baada ya kufunga ndoa hiyo.

“Umepata wapi taarifa? Kumbe wamesharusha! Ndiyo tumetoka kanisani tunajiandaa kwenda ukumbini,” alisema Padri Karugendo ambaye pia huchangia makala katika gazeti hili.
Post a Comment