Binti wa Mugabe kuvidhibiti vyombo vya Habari - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 24, 2017

Binti wa Mugabe kuvidhibiti vyombo vya Habari

Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,amemteua binti yake wa pekee, aliyemaliza masomo yake nchini Singapore, mwenye shahada ya uzamili katika masuala ya usimamizi katika mabenki na fedha, Bona Mugabe-Chikore, kuwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari.
Bona ameteuliwa kudhibiti vyombo hivyo vya habari ikiwemo na sekta ya filamu katika nchi hiyo. Naye Charity Charamba, ambaye ni msemaji wa jeshi la polisi atakuwa moja ya watu katiaka bodi hiyo ya watu 11.
Bodi hiyo ilitangazwa na Waziri wa mambo ya ndani Ignatious Chombo, ikihusisha wawakilishi wa makundi ya makanisa, wataalamu wa sheria na uhasibu na viongozi wa kitamaduni. Shirika la kitaifa la habari limesema bodi hiyo itadhibiti na kukagua vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini na kulenga “matumivi mabaya ya mitandao ya kijamii .
Post a Comment