Naibu Waziri aliyetishiwa na bunduki jana afikishwa Mahakamani Kisutu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 17, 2017

Naibu Waziri aliyetishiwa na bunduki jana afikishwa Mahakamani Kisutu

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, na Mbunge wa Mkuranga, Adam Kighoma Ali Malima amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo akituhumiwa kumzuia Polisi kutekeleza majukumu yake.

Malima anatuhumiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2017 eneo la Masaki karibu na Ubalozi wa Canada jijini Dar es Salaam jana majira ya saa sita mchana, ambapo Polisi walikuta ameegesha gari lake sehemu isiyotakuwa na alipotakiwa kulipeleka ‘yard’ alikataa.

Polisi hao walikuwa wameambatana na maofisa wa kampuni moja ambayo ni wakala wa kukusanya madeni, kukamata teksi bubu pamoja na kukamata magari ambayo yanaegeshwa sehemu ambayo si sahihi kisheria.

Licha ya Malima kuelezwa ukweli kuwa hakuwa ameegesha gari sehemu sahihi, lakini alikataa kulipeleka alikoambiwa jambo lililoibua mtafaruku mkubwa.

Baada ya kufikishwa mahakani yeye na dereva wake, wameachiwa kwa dhamana ya TZS milioni 5.
Loading...

No comments: