UCHAGUZI TFF: Hatua ya mchujo ya mtoa mjumbe wa kanda Kagera na Geita - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 24, 2017

UCHAGUZI TFF: Hatua ya mchujo ya mtoa mjumbe wa kanda Kagera na Geita

Katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.


Makao makuu ya Shirikisho la Mpira Tanzania TFF

Majina 73 yamepita katika hatua ya awali, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imechuja jina la Abdallah Mussa katika orodha ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao wa shirikisho.
Sababu za kukata jina la Mussa ambaye alikuwa anawania nafasi ya Ujumbe kutoka Kanda Na. 1 ya mikoa ya Kagera na Geita ni kutoambatanisha kivuli cha cheti cha kidato cha nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF.
Katika majina hayo 73, majina 10 ni wale wanaowania urais, makamu rais sita na wajumbe wa kamati ya utendaji 57.
Wagombea wote hapo juu wanatakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29, 2017 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA).
Imetolewa na
Alfred Lucas
Ofisa Habari wa TFF
0769 088 111
Post a Comment