Aliyemvamia Mchezaji Wayne Rooney Uwanjani Asamehewa Kwa Amri ya Makamu wa Rais Samia Suluhu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

.

.

Friday, July 14, 2017

Aliyemvamia Mchezaji Wayne Rooney Uwanjani Asamehewa Kwa Amri ya Makamu wa Rais Samia Suluhu


MMOJA wa mashabiki wa Tanzania waliofika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamamejitoa ufahamu na kumvamia mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney kwa nia ya kumkumbatia wakati wa mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ukiendelea uwanjani hapo.
Baada ya kitendo hicho ambacho amekifanya wakati mpira ukiwa umesimama kwa muda kufuatia mmoja wa wachezaji wa Gor Mahiakuumia na kulala chini, polisi walimvaa shabiki huyo na kumwondoa uwanjani humo mpesempese. 
Hata hivyo shabiki huyo ameachiliwa huru kwa amri ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo. (Picha na Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)
Post a Comment