KUONGEZEKA KWA WAHITIMU VYUONI JE? KUNA HAJA YA KUONGEZA/KUJENGA VIWANDA KWENYE VYUO VYETU? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, July 21, 2017

KUONGEZEKA KWA WAHITIMU VYUONI JE? KUNA HAJA YA KUONGEZA/KUJENGA VIWANDA KWENYE VYUO VYETU?

Sebastian Emmanuel jr mwandishi wa makala haya.


Sebastian Emmanuel jr,
 Mafinga, Iringa, Tanzania.
0714761468.
Kama kuna kitu kinanitatiza kwenye mawazo yangu na kunifanya niamini kwamba Tanzania na mataifa ya afrika.
Kwa ujumla ni pale kila mwaka ninaposikia idadi ya wahitimu kwenye vyuo vyetu inapoongezeka mara dufu. Sina takwimu halisi ya wahitimu ambao wamehitimu kwenye vyuo mbalimbali kuanzia 2005 – 206 lakini naamini idada itakuwa ni kubwa mno kwa hapa kwetu Tanzania.
Idadi ni kubwa mno mpaka inalazimu sasa wakuu wa vyuo vingine kufanya sherehe mara mbili kwa mwaka yaani (Graduation) kwani imedhihilika hapa karibu ya tarehe 12/11/2016 siku ya jumamosi, siku ambayo tumemsikia makamu wa mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam yaani UDSM professor Rwekaza Makandala alipokuwa ametoa taarifa ya ongezeko la wahitimu mpaka ikamlazimu kufanya mahafali mara mbili, taarifa ambayo ilinistua mwandishi wa makala hii mpaka nikajiuliza kwani kuna athari gani vyuo vyetu vikianzisha viwanda ambavyo vitasaidia kuajiri hawa wahitimu hata kama sio wote.
Mimi kwa umbumbu wangu ninafikiri sasa kwamba hivi vyuo vyetu vikuu yaani UDSM, UDOM, Mzembe vikaanzisha mchakato wa kila chuo kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaajiri hawa wahitimu hata kama sio wote kwani mimi nafikiri itakuwa na maana zaidi tunapozungumza Tanzania ya viwanda tukazungumza wote kwa pamoja na vyuo vyetu.
Ni vigumu sana kuambatanisha chuo na kiwanda lakini mimi naona kama kutakuwepo mjadala wa wadau wote wa elimu yani serikali, wana vyuo, maprofesa na wataalamu mbalimbali wa sekta ya viwanda. Mimi naona inawezekana kwa sababu mhitimu atakuwa amemaliza masomo yake na chuo ndicho kitakuwa kinamiliki kiwanda, kwa hiyo mimi naona kutakuwa na muingiliano; ukifikiri kwa mazoea utaona chuo na kiwanda ni vitu tofauti sana lakini ukiangalia tatizo la ajira kwa sasa utaona kuna sababu ya kuanzisha mjadala wa pamoja ili tuone kama kuna uwezekano wa kuanzisha hivyo viwanda
Kwa nini muandishi wa makala hii amefikiria vyuo vyetu viwe na viwanda? Sababu ya kwanza naamini kwamba vyuo vyetu ndio chimbuko la wataalam mbalimbali kwa hiyo naamini kwa mchanganuo huo wataalamu ndio itakuwa mafanikio ya hivyo viwanda. Sina elimu ya namna gani chuo kama chuo kinaweza kinaweza kuanzisha kiwanda ndio maana nasisitiza kuwe na mjadala mpana wa wadau wote ili kuangalia ni jinsi gani chuo kinaweza kuendesha kiwanda kwa ajiri ya wahitimu wake, kwani ni mawazo yangu mimi ambaye ni mtu mmoja nikiamini kwamba kuna watu mbalimbali wakiwemo wanavyuo wenyewe wanaweza kuchangia mjadala huu kwani kuna jambo ambalo limnasikitisha pale ninapomuona mkuu wa chuo akikabidhi cheti cha wahitimu zaidi ya elfu sita ambao baadhi yao wanadaiwa na serikali wakati hawajui hilo deni watalipaje
Nawaonea huruma wale vijana nikiwaona wanahitimu masomo nikiwa na uhakika kwamba wanaingia kwenye maisha ya kuangaika ajira ambazo hawana uhakika wa kuzipata iwe ya kujiajiri au kuajiriwa  
Huku kwenye vichwa vyao kukiwa na mawazo mengi wakifikiria ni jinsi gani watapata ajira ili walipe hilo deni ambalo wamekopeshwa na serikali, kwani serikali inamkopesha mtu ambaye hawajui atawalipa lini deni.
Kwa utaratibu wa kuanzisha viwanda vinavyosimamiwa na vyuo vyetu tutapunguza kwa kiasi Fulani ukosefu wa ajira pia litapunguza tatizo la kutorudisha mikopo ya wanafunzi kwa wakati, pia kutawafanya wahadhiri wengi kuingia kwenye mchango wa mapinduzi ya viwanda ambayo serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na mwana viwanda, Rais John Pombe Magufuli na huo ndio utakuwa mchango mkubwa kwa wasomi wetu ambao wanashinda vyuonikwa maana ya wahadhili tofauti na ilivyo sasa ambao wahadhili wetu wanakuwa wachambuzi wa mambo ya uchumi pamoja na siasa na hotuba za viongozi wa kitaifa.
Mimi naamini chuo kikimiliki kiwanda kitakuwa na maana sana kwa taifa letu bila kutolea mifumo ya vyuo vingine vya nje ya nchi yetu. Wao kama hwajaanza wataiga sisi kwani natamani siku moja nimsikie mhadhili akielezea namna ya kiwanda cha chuo kinavyochangia pato la taifa pamoja na ajira
Akizungumza kwenye maafali ya 46, tarehe 12/11/2016 makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Professor Rwekaza Mukandala alisema kuna ongezeko la wahitimu ambao kulilazimu kufanya maafali mara mbili.
Hapo ndipo wazo langu la kuandika makala hii au kutoa wazo langu la siku nyingi ambalo ninajiuliza siku zote, kunaubaya gani hivi vyuo vyetu vikianzisha viwanda. Pia katika mahafali hayo alikuwepo Rais mstafu wa Afrika ya kusini Mh. Thabo Mbeki ambaye alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari.
Akizungumza katika mahafali hayo Mbeki pamoja na mambo mengine alisema changamoto zinazoikabili Afrika kwa sasa ni kuchangia maendeleo ya uchumi na viwanda. Hata hivyo Mbeki alisema ajenda za utafiti wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu barani Afrika vimejielekeza katika madhumuni ya sayansi na taaluma na kiasi kidogo cha mahitaji ya maendeleo kwa maelekezo ya Mbeki yalinipa matumahini ya kuanzisha mjadala   mpana wa kuona kwamba kuna umuhimu wa vyuo vyetu kuanzisha viwanda kwa ajili ya kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu.
Mimi naamini inawezekana, sijui wenzangu watachukulia vipi wazo langu hilo, ndio maana napenda niwasikie wasomi wenyewe wanasemaje; kuhusu wazo langu hilo.
Mimi naamini hata siku moja maneno tupu hayabadilishi dunia bali vitendo ndio vinaweza kubadilisha dunia.
Tunasubiri viwanda bila kuumiza vichwa vyetu
Sababu nyingine ambazo zimefanya nizidi kujidhatiti kwenye wazo langu la vyuo kuanzisha viwanda ni pale nilipo amka mapema siku ya taerhe ………………. Na kukimbilia kwenye vituo vya kuuza magazeti na nikakuta vichwa vya habari vya magazeti yameandikwa tena kwa kukolezwa wino moja wapo liliandika MIKOPO ELIMU YA JUU WADAU 142,470 WAPEWA SKU 30 KULIPA MADENI – TRILIONI 3/=ZA KOPESHWA TANGU MWAKA 1995, taarifa hii kutoka kwa bodi ya mikopo ilinipa nguvu ya kuandika makala hii na nikazidi kuwaza huku nikijiuliza sijui hawa wadaiwa walisha wahi kuajiriwa sehemu yoyote wakapata pesa za kurudisha kwenye bodi ya mikopo
Taarifa nyingine ambayo nilikuwa sijui ni pale niliposikia kuwa baada ya kumaliza masomo mhitimu anapewa siku 365 yaani (miezi 12 tu ) ili aanze kurudisha mikopo.Taarifa pia ilinipa nguvu pia ya kuandika makala hii kwa sababu kwa hali ilivyo hivi sasa na tatizo kubwa la ajira. Sioni uwezekano wa muhitimu atapata kazi iwe ya kujiajiri au kuajiriwa mwenyewe, kwa muda wa miezi 12 hapo ndipo ninamuonea huruma muhitimu kwa sababu anaingia madeni akiwa na maswali mengi yasiyo na majibu, huku akiwa tayario ana deni ambali hajuwi atalipaje.
Hapo ndipo nawauliza wadau kuongezeka kwa wahitimu kwa vyuoni je? kuna haja ya vyuo vyetu kumiliki viwanda?


Post a Comment