Rais Magufuli Awapongeza Watanzania Kwa Kujitokeza kwa Wingi Kulipa Kodi ya Majengo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

.

.

Saturday, July 1, 2017

Rais Magufuli Awapongeza Watanzania Kwa Kujitokeza kwa Wingi Kulipa Kodi ya MajengoSeeBaitRais John Magufuli amewapongeza Watanzania kwa mwamko waliounyesha wakati wa ulipaji wa kodi ya majengo.
Akizungumza leo (Julai 1) wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Rais amesema  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilipochukua jukumu la kukusanya kodi hiyo imewezesha wananchi kulipa kodi kwa amani.
“Walipochukua TRA, sasa waliwathaminishia kodi ambayo wananchi wanaweza kuilipa, ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi. Haijapata kutokea wananchi wakataka kulipa kodi kwa kiasi kile, ni kwa sababu ilikuwa nafuu kwao,” amesema
Pia, Rais amewataka TRA kuendelea kukusanya kodi kwa njia ambazo ni rafiki kwa kuwa wananchi hawapendi kodi inayowaumiza bali kodi ambayo ni sahihi kwao.
“Wananchi wanapenda kulipa kodi  lakini iwe na manufaa kwako,” amesema
Post a Comment