ROSE TWEVE, WANAWAKE TUTHUBUTU. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

.

.

Saturday, July 1, 2017

ROSE TWEVE, WANAWAKE TUTHUBUTU.

   
 mbunge Rose Tweve  akizungumza mbele ya wanawake wa kata ya Nyololo walio fika kumsikiliza na kukabidhiwa pesa taslimu shilingi laki tano na laki moja ataweka kwenye account zao za kikundi cha wanawake wajasilia mali.
 wanawake wa kata ya Nyololo wakishangia pamoja na Mbunge Rose Tweve wakati akiwakabidhi pesa wakati wa uanzishwaji wa kikundichao cha kijasiliamali.

 wanawake wa kata ya Malangali wakimlaki mbunge wao wa viti maalumu alipofika katani hapo
 mbunge Rose Tweve akisalimiana na wazee waasisi wa chama cha Tanu na mapinduzi (pamoja na picha ya chini)

 Mbunge RoseTweve akikabidhi pesa shilingi laki sita na laki moja anaweka kwenye bank account yao, kwa wanawake wajasilia mali ambao wameamua kwa pamoja kuanzisha duka la pembejeo za kilimo
 Mbunge Rose Tweve akioa neno la shukrani mara baada ya kupewa zawadi

                                             
Na Sebastian Emmanuel, Mufindi.
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (ccm) mkoa wa Iringa, Mh. Rose Tweve amewataka wanawake wote nchini kujiamini na kuthubutu kufanya maamuzi sahihi katika Nyanja mbalimbali za kiuongozi, amewaomba wanawake kuto kubaki wakilalamika badala yake wachukue hatua za kuungana na kuaminana hasa kwenye uchumi, siasa, kilimo, elimu na afya kupitia vikundi mbalimbali vya kiujasiliamali vya wanawake.
Rose Tweve  ambaye mpaka sasa amezunguka katika kata 49 za mkoa wa iringa amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaelimisha wanawake kuungana ili kuweza kufanikiwa kuzishinda changamoto za kimaisha ambazo zimekuwa kikwazo kwa wanawake wengi mkoani hapo na Tanzania kwa ujumla.
Wiki hili Mh. Rose Tweve ametembelea kata saba (7) za wilaya ya Mufindi jimbo la Mufindi Kaskazini na kukutana na wananchi/wanawake kata hizo ni pamoja na Idunda, Maduma, Nyololo, Malangali, Mtambula, Kasanga, na Igowole ambapo wanawake wote wa kata hizo wameunda vikundi vya kijasilia mali na kupewa kila kata shilingi laki sita kwa ajili ya kuanzishia mtaji na pesa hizo wamepewa bila kulipa gharama zozote kwa mbunge huyo.

Aidha wanawake hao wamemshukuru Mbunge huyo kwa moyo wake wa kuwajali kwani haijawahi tokea tangu nchi hii kupata  uhuru mbunge wa viti maalumu kuwatembelea na kuwapa mitaji tena bila riba yoyote.      
Pia wanawake hao wamemuahidi mbunge huyo kuto muangusha na kwa kuwa tayari baadhi yao wameshaanzisha biashara katika vikundi vyao vya kijasiliamali.
Post a Comment