Fahamu Hapa Kuhusu "Blue Ticks" kwa watumiaji wa whatsapp Ni Nomaaa Sasa Ule Uongo utaisha - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, November 8, 2014

Fahamu Hapa Kuhusu "Blue Ticks" kwa watumiaji wa whatsapp Ni Nomaaa Sasa Ule Uongo utaisha


Kuanzia jana longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa mchana kweupe.
  • Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia 
  • Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
  • Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
  • Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
  • Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
whatsapp
Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo ambayo yamewakera baadhi ya watumiaji.
Kuanzia jana huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.

No comments: