WhatsApp yavunja ndoa! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 19, 2015

WhatsApp yavunja ndoa!


Mtandao wakijamii wa WhatsaApp umesababisha ndoa moja kuvunjika nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa habari hiyo iliyoandikwa katika gazeti la Al-Hayat, Mahakama nchini Saudi Arabia imeshuhudia kwa mara ya kwanza kesi kuhusiana na WhatsApp kusababisha ndoa kuvunjika baada ya mwanaume ambaye alimshitaki mkewe mahakamani kuonesha sababu ya kutaka kuachana na mke wake huyo ni status aliyokuwa ameiandika WhatsApp ikisomeka "Ninaomba dua kuwa na subira na uvumilivu kwako."

Mwanamme huyo alieleza kuwa yeye amekua mnyenyekevu sana kwa mkewe na kwamba hali hiyo haikuanza leo na haoni maendeleo yoyote mazuri ya ndoa yao.

via TRT Swahili

No comments: