Bado Nitaendelea Kufanya Muziki - Professor Jay12080694_899379490146509_1446453151_n
Mbunge mteule wa Mikumi kipitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Haule aka Professor Jay, amesema ataendelea kufanya muziki hata akiwa bungeni kwa sababu ndio kitu kilichomfikisha hapo alipo.

Professor amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa ataendelea kukiheshimu kipaji chake licha ya kupata tiketi ya kuingia bungeni.
“Muziki niliokuwa nikiufanya na ninaoendelea kuufanya ni sauti ambayo nilikuwa nikiipaza kwa ajili ya ustawi wa taifa langu na mustakabali wa nchi yangu. Nimeimba vitu vingi kuhusiana na changamoto zinazotukabili katika maisha yetu, so muziki umefanya niweze kupata sauti na kusikika zaidi,” amesema.
“Kwahiyo muziki umeplay role kubwa ya mafanikio haya maana nisingejulikana bila muziki, nitaendelea kuheshimu muziki na ni kipaji ambacho nimepewa na Mungu hata kama naingia mjengoni nitaendelea kufanya muziki,” ameongeza.

Post a Comment

0 Comments