Chelsea waweka wazi, klabu iliyoweza kumnunua Oscar - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, December 23, 2016

Chelsea waweka wazi, klabu iliyoweza kumnunua Oscar


Mchezaji raia wa Brazil, Oscar anayekipiga katika klabu ya Chelsea nchini Uingereza anategemewa kuihama klabu ya Chelsea katika dirisha la usajiri la mwezi wa kwanza 2017. Hii ikiwa ni baada ya miezi 12 ya mchezaji mwenzie wa  taifa la Brazil Ramires aliyekua anacheza katika klabu ya Chelsea alipojiunga na timu ya Jiangsu Suining ya huko china.

Klabu ya chelsea imeweka wazi uamisho wa Oscar mapema leo asubuhi. Oscar ni mchezaji anayecheza sehemu ya kiungo. Hapo januari atajiunga na klabu ya Shanghai Bridge kwa ada ya Paundi milioni 60.

Meneja wa Oscar katika klabu yake mpya ya Shanghai ni kocha wake wa zamani wa klabu ya Chelsea, bosi Andre Villas-Boas.


Loading...

No comments: