Haya ndio yaliojiri kwenye mchezo wa Yanga na Ndanda FC - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, December 28, 2016

Haya ndio yaliojiri kwenye mchezo wa Yanga na Ndanda FC


Timu ya soka ya Yanga ilishuka dimbani kupambana na Ndanda Fc yakutoka Mtwara, na kuweza kuigaragaza Ndanda kwa kipigo kikali zaidi mbele ya Yanga tangu timu ya Ndanda Fc ipande daraja.

Goli la kwanza limefungwa na Dornad Ngoma dakika ya 8 ya mchezo. Ngoma aliiandikia Yanga goli la kwanza na baadae dakika ya alirudi tena kuzichana nyavu za ndada na kuandika goli la pili.

Goli la tatu limefungwa na Hamis Tambwe ambalo ndio goli lake la 9 katika msimu huu kuifungia Yanga. Yanga imemaliza kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza jumla ya magoli 3 - 0.

Goli la 4 la Yanga limefungwa na Bossou katika dakika ya 89. huku likiwa goli lake la pili katika msimu huu.
Loading...

No comments: