Mourinho atupilia mbali umri wa Zlatan Ibrahimovic - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 25, 2016

Mourinho atupilia mbali umri wa Zlatan Ibrahimovic


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden amekua akizungumziwa sana Old Trafford, kwakufunga magoli 16 katika mechi 25 za klabu ya Manchester United.

Ibrahimovic amekua akihusishwa na taarifa zakuondoka Uingereza na kwenda kujiunga na klabu za Marekani au China, ambazo zilikuwepo kabla hajajiunga na Manchester United.

Kocha Mourinho  alipohojiwa na Sky Sports amenukuliwa  
“I’m really happy for him. Maybe some people thought he was a top scorer but not anymore at 35 years old. But for him, 35 is the same as 25, Ligue 1 is the same as the Premier League".

"Nafuraha sana kwa Zlatan. Inawezekana watu wanafikiria ni moja kati ya wafungaji bora lakini hawezi fanya hivyo akiwa na miaka 35. Lakini kwa Zlatan, umri wa miaka 35 ni sawa na miaka 25, Ligi ya Ufaransa ipo sawa na ligi ya Uingereza"

Kocha amesema Zlatan kwa sasa amekua bora sana kuliko nilipokua naye pale awali. Mourinho alishinda kombe la Ligi ya Italia akiwa na Zlatan, mwaka 2009 ndani ya kikosi cha Inter Millan.

Mourinho amesema alikua na Zlatan akiwa na umri wa miaka 25, 26 na  27 kwa muda mchache lakini kwa sasa nampenda maana anafanya vizuri zaidi.

Zlatan atamaliza soka lake atamaliza akiwa na klabu ya Manchester United, kocha kasema baada ya kupata sahihi ya Zlatan akipo ihama klabu ya Paris ya Ufaransa.

Loading...

No comments: