Professor Jay Amuandikia Barua Yenye Ujumbe Mzito Darassa. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, December 15, 2016

Professor Jay Amuandikia Barua Yenye Ujumbe Mzito Darassa.Ni ukweli kuwa kwa sasa Darassa ameyasogelea mafanikio aliyokuwa akiyatamani kwa muda mrefu. Rapper mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Professor Jay amemuandikia ujumbe hitmaker huyo wa Muziki wa kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka kuendelea kukaza buti.

Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameandika:

Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP,
SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS
#ACHA MANENO WEKA MUZIKI
@darassacmg @darassacmg
Loading...

No comments: