Real Madrid yatwaa taji la dunia; Ronaldo apiga tatu kwa mpigo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, December 18, 2016

Real Madrid yatwaa taji la dunia; Ronaldo apiga tatu kwa mpigo


Mchezo wa fainali wa klabu bingwa wa dunia umechezwa katika uwanja wa Nissan mchana huu. Mechi ilikua kati ya Real Madrid vs Kashima Anters. Dakika 90 matokeo yalikua ni mabao 2 -2 , Zikaongezwa dakika30 ambapo Ronaldo alifunga magoli mawili dakika ya 97 na 104 na kufanya Madrid kupata ushindi wa mabao 4 - 2.


Ronaldo amefunga jumla magoli matatu katika dakika ya 60. 97 na 104. Goli l;a kwanza la Madrid limefungwa na Benzema dakika ya 9.

Magoli mawili ya Kashima yamefungwa na Shibasaki dakika ya 44 na 52.

Modrick kapewa tuzo ya shaba kama mchezaji bora wa pili katika mashindano.
Ronaldo kapewa tuzo ya dhahabu kama mchezaji bora.


Loading...

No comments: