Ronaldo agoma kuhamia China - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, December 31, 2016

Ronaldo agoma kuhamia China

Ronaldo wakati akisaini mkataba wake mpya mwezi Novemba na klabu ya Real Madrid alisema anaweza cheza soka kwa miaka 10 zaidi mbeleni. Ambapo mkataba mpya na Real Madrid utakoma Juni 2021.

Wakala wa mchezi bora wa dunia Ronaldo, bwana Jorge Mendes ameweka wazi kua nahodha wa timu ya taifa ya Ureno mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa hana mpango wakuhamia katika klabu ya china.

Hii ofa imekuja baada ya klabu ya Shanghai Shenhua kutoka china kukamilisha usajili wa Carlos Tevez kutoka klabu ya Boca Juniors; ndipo nguvu ya pesa ikahamia kwa Ronaldo.

Klabu ya Shanghai Shenhua, inataka kumlipa Ronaldo kiasi cha paundi milioni 1.6 ikiwa ni mara tatu zaidi ya ada ya uhamisho ya mchezaji wa Man United, Pogba ya paundi milioni 89 akitokea Juventus.

Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendez ameweka wazi kwamba mteja wake Ronaldo angweza kwenda kujiunga na klabu ya Shanghai na kulipwa Euro milioni 100 kwa mwaka. Lakini Ronaldo amechagua kubaki katika klabu ya Real Madrid.
Loading...

No comments: