Video: Trey Songz akifanya uharibifu wa jukwaa; anashikiliwa na polisi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, December 30, 2016

Video: Trey Songz akifanya uharibifu wa jukwaa; anashikiliwa na polisi

Mwimbaji mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa, mnamo tarehe 28 Disemba, mkali wa miondoko ya RnB mwanamziki Trey Songz ambaye jina lake kamili ni Tremaine Neverson. Amekamatwa na polisi baada ya uovu wa uharibifu wa vifaa na pamoja na kukataa kushikiliwa na polisi.

Tukio limetokea huko Detroit katika tamasha la Joe Louis Arena, wakati Trigga akiwa yupo jukwaani akitumbuiza. Baada ya kutumbuiza na kupiliza muda aliopangiwa kuwa jukwaani, baada yakuambiwa amalize/ aikatishe show hapo ndipo Trey Songz akapatwa/ akaingiwa na jazba.

Trey Songz aliruka kwenye umati wa mashabiki baada ya taa kuzimwa.

Trey Songz alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Detroit 36th katika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Disemba. Hakimu alitaja dhamana yake ni dola za kimarekani $25,000 au asilimia kumi.

Kwa uharibifu aliofanya anaweza akapata adhabu ya kwenda jera miaka 4 pamoja na faini ya mpaka dola 5000 kwa hujuma kwa askali wa usalama.

Trey Songz atarudishwa mahakamani Januari 5, muda 8:30 asubuhi.


Loading...

No comments: