Arsene Wenger hana malengo yakusajili mwezi Januari - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 2, 2017

Arsene Wenger hana malengo yakusajili mwezi Januari


Arsenal wamerudi kwenye makali yao katika michezo ya wiki zilizopita baada yakufuruliza kwa kupata ushindi, Arsenal kwa sasa wapo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi huku wakiwa wameachwa alama 9 na klabu ya Chelsea ambao ni vinara wa ligi kuu ya Uingereza kwa sasa.

Arsenal imekua ikihusishwa na taarifa zakuwasajili wachezaji tofauti katika majira ya mwezi wa kwanza, taarifa zakuwasajili Ross Barkley, Julian Brandt na Franck Kessie. Lakini Wenger hatarajii kusajili katika dirisha la usajili kipindi cha baridi na badala yake atafanya kuwarudisha washambuliaji walio umia katika speed ya kubwa.

Bosi wa Arsenal, Arsene Wanger alidai kuwa anafuraha na ubora wa kikosi cha Arsenal na kwasasa hana lengo lakufanya mabadiriko mapya katika dirisha lausajiri la Januari.

"Hakuna kitu nilichopanga kwa kipindi hiki," aliwaambia BBC sport baada ya kupata ushindi wa 2 - 0 dhidi ya Crystal Palace siku ya jumapili jioni. "wewe unaangalia katika wachezaji waliokosekana leo, hakuwepo Saint Cazora na Mesut Ozil, tunaimani yakuwarudisha dimbani. Danny Welbeck anarudi. Tunakikosi kikubwa"
Loading...

No comments: