Mayanja: Simba wapeleka moto kombe la Mapinduzi Zanzibar - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 2, 2017

Mayanja: Simba wapeleka moto kombe la Mapinduzi Zanzibar


Mwaka 2016 klabu ya Simba imemaliza ikiwa inaongoza ligi ya Tanzania bara, hii hali imewafanya mashabiki kua na furaha katika kufunga mwaka 2016 na kuanza mwaka 2017.

Simba kwa sasa imeelekea Zanzibar kwaajili yakushiriki kombe la Mapinduzi. Klabu ya Simba ina hamu kubwa sana yakutwaa kombe la Mapinduzi pamoja na ligi kuu ya Tanzania ambavyo ni moja ya vipao mbele vyao vikuu.

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amewaambia wanachana na mashabiki wa Simba wajitokeze kwa nguvu kuiunga mkono timu yao kwaajiri yakuongeza mori zaidi katika speed waliyoanza nayo katika mashindano ya ligi kuu katika mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Kikosi cha Simba kilichoenda kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi kinaundwa na 
makipa: Peter Manyika, Dennis Richard na Daniel Agyei.
Mabeki ni Hamad Juma, Janvier Bokungu, Novaty Lufunga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda na Method Mwanjali.
Viungo ni Said Ndemla, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Muzamil Yassin, James Kotei na washambuliaji Pastory Athanas, Juma Luizio, Mavugo na Blagnon.

Loading...

No comments: