Mwana FA: Mwaka 2017 Hautakufanyia Chochote Kama Hauna Mipango. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 2, 2017

Mwana FA: Mwaka 2017 Hautakufanyia Chochote Kama Hauna Mipango.


Imezoeleka kila mwaka unapaonza watu huwa na hamasa na hali ya kuona wanafanya mageuzi katika maisha yao katika vitu mbalimbali huenda katika kazi, maisha kiujumla na wengine wakiweka malengo na kuona wanatimiza kabla ya mwaka kuisha lakini
wengi wao hamasa na ile hali ya kutekeleza kile alichopanga huwa inaanza kushuka kadili siku zinavyozidi kwenda na kujikuta anaingia mwaka mwingine akiwa hajatekeleza kile alichopanga.
Kutokana na hali hiyo Rapa Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Dume Suruali' amefunguka na kuwakumbusha watu kuwa katika kuanza huu mwaka mpya 2017 kama hutakuwa na mpango mathubuti na yenye kueleweka utakuwa ni mwaka wenye mabadiliko tu ya tarehe lakini si mwaka wenye kuleta tija katika maisha yako, hivyo unapaswa kujipanga kwa mipango zaidi na kuona hiyo mipango inafikiwa ili kuleta tija.
"2017..haimaanishi utakufanyia Chochote kama huna mipango ya kueleweka..Utakuwa ni mabadiliko tu ya tarehe..FOCUS..Heri ya mwaka mpya" aliandika Mwana FA.
Loading...

No comments: