Obi Mikel amethibitisha kuhamia China - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 7, 2017

Obi Mikel amethibitisha kuhamia China


John Obi Mikel ni raia wa Nigeria anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza. Obi Mikel anacheza nafasi ya kiungo wa katikati katika timu yake yataifa ya Nigeria.

John Obi Mikel ametangaza katika ukurasa wake wa Twitter kwamba atajiunga na klabu ya Tianjin TEDA ya nchini China.

Hii inakuja baada ya wachezaji wenzake wa klabu ya Chelsea kuhamia China, Oscar amejiunga na Shanghai SIPG  na Ramires ambaye alihama klabu ya Chelsea mwaka jana.

Mikel anaihama Chelsea kwasababu hajapata nafasi yakutosha kuicheza katika timu kwa msimu huu. Obi amekua akikaa benchi. Obi anamiaka 29 kwa sasa na amesema yeye bado umri wake unamruhusu kucheza soka kwa miaka mingi mbeleni.

Mshahara wake mpya utakua EURO 400,000 kwa wiki.

Loading...

No comments: