Simba yaanza kwa makeke Mapinduzi Cup - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 2, 2017

Simba yaanza kwa makeke Mapinduzi Cup


Mchezo wa kwanza wa Simba, umechezwa katika uawanja wa Amaani mjini Zanzibar ikiwa inakutana na timu ya Taifa Jang'ombe jioni ya leo tarehe 2 mwezi januari 2017.

Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2 - 1. Simba walipata bao la kuongoza katika dakika ya 28 kupitia kwa Muzamiri Yassin, mpaka mapumziko Simba 1 - 0 Taifa Jang'ombe.

Kipindi cha pili, Beki wa simba Noverty Lufunga alipata bahati mbaya baada ya kujifunga goli baada ya kuunganisha mpira wa kona.

Mabao 2 ya Simba yamefungwa na Muzamiru pamoja na Juma Luizio.

Katika mechi ya ufunguzi Taifa Jang'ombe ilishinda 1 - 0 dhidi ya Jang'ombe Boys katika mchezo waufunguzi uliofanyika tarehe 30 disemba 2016.


Loading...

No comments: