Barakah The Prince aingia kwenye kilimo cha mboga mboga - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 26, 2017

Barakah The Prince aingia kwenye kilimo cha mboga mboga

Muimbaji wa muziki Barakah The Prince amedai kwa sasa ameamua kuingia kwenye biashara ya kilimo ili kuwa na kipato nje ya muziki.
Akiongea katika cha kipindi cha Twenzetu cha Times Fm, Barakah amedai nje ya muziki ameamua kijikita kwenye kilimo cha mboga mboga.
“Nina shamba Morogoro na Tarime,Tarime nimelima Matikiti maji na Morogoro nimelima Vitunguu ,Kabichi na Mboga Mboga , bado sijaanza kuvuna ni shanba ambalo nimelikodisha kama miezi miwili hadi sasa ,Masanja ndio alinishawishi kuingia katika masuala ya kilimo.” alisema Barakah.
Muimbaji huyo alisema hayo alipotembelea kutuoni hapo kuutambulishwa wimbo wake mpya ‘Acha Niende’ ambapo aliambatana na mpenzi wake Naj.
Loading...

No comments: