Fifa ya mfungia maisha refa wa Ghana - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 21, 2017

Fifa ya mfungia maisha refa wa Ghana


Refa ambaye ni raia wa Ghana Joseph Lamptey, amefungiwa maisha na shirikisho la kandanda Duniani Fifa, baada ya masuali kuibuka jinsi alivyosimamia mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Senegal na Afrika Kusini Novemba 2016, iliyopita.

Joseph Lamptey
Afrika Kusini ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1 lakini Senegal ikalalamika kwa shirikisho la Fifa.
Walisema kuwa Lamptey aliwapa Afrika kusini penalti licha ya naibu refa kuashiria kuwa ingekuwa kona.
Wengi waliuliza maswali kuhusu kona hiyo wakati huo, kikiwemo kitengo cha michezo cha BBC kilichoripoti kuwa Afrika Kusini iliongoza baada ya panelti hiyo yenye utata.
Loading...

No comments: