Mohammed Ali wa Jicho Pevu Aastaafu Kufanya Habari za Uchunguzi na Kufichua Maovu.. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 6, 2017

Mohammed Ali wa Jicho Pevu Aastaafu Kufanya Habari za Uchunguzi na Kufichua Maovu..Mwandishi Mahiri wa Habari za Uchunguzi, Mohammed Ali anayefahamika kwa Makala za Jicho Pevu ametangaza kujiuzulu kutoka taaluma ya kufichua maovu ya kiutawala na jamii na kujiunga na siasa.

Mohammed katika mtandao wake wa Twitter ameandika "Kwa miaka 10 mfululizo nimekuwa nikisimama nanyi kuzidisha sauti zenu za kuangaishwa. Sasa ni wakati wangu wa kuwauliza, msimame nami katika harakati zangu za kuwania ubunge wa Nyali kwa tiketi ya ODM". Ameahidi kuwa akitimiza ndoto hiyo atakuwa mshirikishi mkuu wa utawala wa haki kwa Wakenya wote bila ubaguzi.
Loading...

No comments: