TASWIRA; KAMA ULIKOSA KUONA MECHI YA YANGA NA ZANACO, JIONEE HAPA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 11, 2017

TASWIRA; KAMA ULIKOSA KUONA MECHI YA YANGA NA ZANACO, JIONEE HAPA

Na Zainab Nyamka.


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, "Dar Young Africans" wameshindwa kutamba kwenye kiwanja cha nyumbani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco ya Zambia uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ulioanza saa 10 alasiri, ilikuwa ni Yanga iliyowachukua dakika 38 kuandika goli  la kwanza kupitia kwa Simon Msuva akiifungia goli la kuongoza akipokea pasi ya Justine Zulu.
Yanga walishindwa kutumia nafasi walizozipata na mpaka kufikia mapumziko Yanga wanaenda wakiwa kifua mbele.
Kipindi cha Pili kinaanza kwa kila upande kulishambulia goli la mwenzake, hali iliyompelekea Kocha George Lwandamina kufanya mabadiliko kwa kumtoa Donald Ngoma na Thaban Kamosoku na kumuingiza Juma Mahadhi na Emanuel Martin.
Katika Dakika ya 82, Atram Kwame anaisawazishai Zanaco wakitumia mwanya wa kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga.
Mpaka dakika tisa zinamalizika Yanga 1-1 Zanaco ambapo mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa kati ya Machi 17-19.
 Kikosi cha Yanga. Kikosu cha Zanaco.


       PICHA NA HABARI KWA HISANI YA http://www.mtaakwamtaa.co.tz          
Loading...

No comments: