Jukwaa la Wahariri (TEF) Lamkaa Koo Profesa Ibrahim Lipumba......Lamtaka Atoe Maelezo Sakata la CUF Kuvamiwa na Waandishi Kupigwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 27, 2017

Jukwaa la Wahariri (TEF) Lamkaa Koo Profesa Ibrahim Lipumba......Lamtaka Atoe Maelezo Sakata la CUF Kuvamiwa na Waandishi Kupigwa

Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) limelaani kitendo cha waandishi wa habari kujeruhiwa katika tukio la uvamizi lililotokea katika mkutano wa CUF katika hotel ya Vina kata ya Mabibo ambapo waandishi wa habari walipigwa na kujeruhiwa

Katika taarifa hiyo ya (TEF) imemtaka Profesa Lipumba kujitokeza na kukiri na kuomba radhi kwa waandishi wa habari pamoja na Watanzania kufuatia tukio hilo kama alivyofanya Maalim Seif

"Tunamtaka Profesa Lipumba binafsi atoe kauli kuhusu tukio hili kama alivyofanya Maalim Seif ambaye binafsi aliandika barua rasmi kwa uongozi wa TEF akilaani kupigwa kwa waandishi wa habari na kutoa pole kwa wale waliomizwa na kupata mshtuko" Walisema viongozi wa TEF

Taarifa hiyo ya TEF ilikwenda mbali zaidi na kuwatahadharisha waandishi wa habari, wahariri kuwa wanapaswa kuwa makini pindi wanapokuwa wanaitwa na kundi hili la Lipumba kwa ajili ya kutoa habari zao 


Advertisement
==
Loading...

No comments: