Lazio yaingia fainali ya Copa Italia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 5, 2017

Lazio yaingia fainali ya Copa Italia

klabu ya Lazio imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya kombe la Copa italia licha ya kufungwa na As Roma kwa 3-2 katika mchezo wa nusu fainali ya pili.
Mchezo wa nusu fainali ya kwanza Lazio walishinda kwa mabao 2-0. Hivyo wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3.
Roma walipata mabao ya kupitia kwa Stephan El Shaarawy katika dakika ya 44, kisha Mohamed Salah akaongeza mengine mawili katika dakika ya 66 na 90.
Mabao ya Lazio yalifungwa na kiungo Sergej Milinkovic-Savic na bao la pili likifungwa na mshambuliaji Ciro Immobile
Nusu fainali ya pili ya kombe la Copa itachezwa leo kwa Napoli kuwaalika Juventus katika dimba la San Paolo.
Loading...

No comments: