Mwakyembe : Basata simamieni shindano la Miss Tanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 28, 2017

Mwakyembe : Basata simamieni shindano la Miss Tanzania
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, HARRISON MWAKYEMBE.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa ufanisi na kuhakikisha waandaaji wanazingatia kanuni za mashindano hayo kikamilifu.

Mwakyembe alisema hayo jana mjini Dodoma wakati alipokutana na Kamati ya Miss Tanzania iliyoongozwa na Hashim Lundenga na kuwataka kusimamia vyema shindano hilo ili kupata washindi wenye viwango vinavyotakiwa kimataifa.

“Nawaagiza Basata simamieni shindano hili ili tupate washindi wenye viwango watakaosaidia Tanzania kujitangaza kimataifa katika tasnia ya urembo,” alisema Mwakyembe.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Muingereza, alimuahidi waziri huyo kuwa atasimamia kwa karibu na kwa ufanisi shindano hilo ili lifanyike kwa ubora utakaowezesha nchi kupata mwakilishi atakayefanya vyema kwenye mashindano ya dunia.

Naye Lundenga aliahidi kushirikiana na wizara hiyo kuboresha shindano la Miss Tanzania ili kuwa na mvuto ambao utaliletea taifa heshima.

Lundenga na wajumbe wengine wa kamati hiyo ambao ni pamoja na Bosco Majaliwa ( Katibu) na Deo Kapteni wanatarajia kuendesha shindano hilo mwaka huu kuanzia ngazi za awali hadi taifa.
Loading...

No comments: