OXFAM TANZANIA WAZINDUA MRADI WA KUKUZA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI KUPITIA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 28, 2017

OXFAM TANZANIA WAZINDUA MRADI WA KUKUZA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI KUPITIA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la kimataifa la Oxfam Nchini Tanzania Bw. Francis Odokorachi akitoa neno la ufunguzi wakati wa  uzinduzi wa mradi wa kukuza utawala bora na uwajibikaji kupitia Teknolojia ya kidijitali
Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Oxfam Betty Malaki akieleza kwa wadau(hawapo pichani)  namna mradi huo utakavyofanya kazi na kuwa umedhaminiwa na Serikali ya Ubelgiji ambao utawagusa zaidi wanawake na vijana
 Kefar Mbogela ambaye alikuwa muwezeshaji katika uzinduzi wa mradi huo wa kukuza utawala bora na uwajibikaji kupitia Teknolojia ya kidijitali akiendelea kutoa mwongozo
 Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ubelgiji Bw. Joris Becker akielezea sababu za kuchagua Shirika la Oxfam kufanya nao mradi huo wa kukuza utawala bora na uwajibikaji kupitia Teknolojia ya kidijitali
Mratibu wa Mawasiliano ya kidijitali kutoka Oxfam  Bill Marwa akielezea namna teknolojia ya kidijitali itakavyotumika katika mradi huo.
 Mmoja wa Muwasilisha Mada Bi. Maria Sarungi akielezea nguvu za mitandao ya kijamii na jinsi inavyoleta mabadiliko katika jamii.
Bwana Richard Mabala kutoka TAMASHA akielezea kwa kina juu ya Uraghbishi 'Active Citizens' ili kuwapa uwelewa zaidi wadau ambao watahusika na mradi huu wa kukuza utawala bora na uwajibikaji kupitia Teknolojia ya kidijitali
 Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hayo.
Mwakilishi kutoka LHRC akizungumza mambo mbalimbali yanayohusu haki za Binadamu
 Baadhi ya wadau wakitoa maoni na kuuliza maswali wakati wa uzinduzi wa Mradi huo
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania


Shirika la Kimataifa la Oxfam Nchini Tanzania imezindua mradi wa miaka miwili wenye nia ya kukuza utawala bora na uwajibikaji nchini kupitia Teknolojia ya kidijitali.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Bw. Francis Odokorachi akitoa maneno ya utangulizi katika uzinduzi wa mradi huo wa miaka miwili alisema mradi huo  utahusisha mikoa mine ambayo ni Geita, Arusha, Mtwara na Kigoma, ambao watapewa simu 200 za kisasa ‘Smartphone’ ambazo zitatumika kutoa taarifa kiwa ajili ya kukuza utawala bora  na uwajibikaji nchini ,alisema kupitia mradi huo wanatarajia kuwafikia watu 50 katika kila Mkoa. 

"Watakaopatiwa simu hizo ni waraghibishi  200 waliokuwa  Katika mradi wa Chukua Hatua ambao watapatiwa mafunzo  katika mradi huo  kuhusu sera, utawala bora, kuhusu wajibu wa wananchi na Serikali,"alisema Odokorachi.

Aliongeza kwamba kupitia teknolojia hii ya kidijitali itaongeza kasi ya utawala bora lwa vijana na watu mbalimbali katika jamii ambapo katika mradi wa Chukua Hatua ulikuwa ni mradi wa wananchi ambao walikuwa wakiibua mambo mbalimbali katika maeneo waliopo kuhusu masuala ya kijamii, utawala bora, ukatili wa kijinsia na mengineyo na viongozi kuweza kuchukua hatua katika changamoto zilizokuwa zinaibuliwa.

Kwa Upande wake  Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Oxfam, Betty Malaki alisema mradi huo umedhaminiwa na Serikali ya Ubelgiji ambao utawagusa zaidi wanawake na vijana.

 “Matokeo ya mradi huo ni sauti za wananchi kuhusu uwajibikaji na masuala mbalimbali kwa uharaka zaidi na kuwafikia wengi kwa muda mfupi”. Alisema Malaki.

Naye Ofisa wa TCRA alisema kuongezeka kwa watumiaji wa mtandao nchini  kumewezesha kuwepo kwa matatizo ya kimtandao ikiwemo ulaghai na utapeli ambao zaidi ni wizi wa fedha mtandaoni na mara nyingi simu na barua pepe hutumiwa zaidi.

Loading...

No comments: