Rais Magufuli awaapisha Makatibu Wakuu, Mabalozi na Kamishna wa TRA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 5, 2017

Rais Magufuli awaapisha Makatibu Wakuu, Mabalozi na Kamishna wa TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu wakuu, Mabalozi pamoja na Kamishna wa TRA, Ikulu jijini Dar es salaam.

Kamshna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Charles Edward Kichele, Balozi wa Tanzania nchini India Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Sylvester Ambokile Mwakinyuke, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Ave Maria Semakafu, Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitilia Alexander Mkumbo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakisoma na kusaini Hati ya kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa na Rais Ikulu Jijini Dar es salaam

Walioapishwa ni pamoja na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Charles Edward Kichele, Balozi wa Tanzania nchini India Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Sylvester Ambokile Mwakinyuke, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Ave Maria Semakafu, Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitilia Alexander Mkumbo.
Loading...

No comments: