Thiery Henry: Ozil asingepata nafasi kwenye Arsenal yangu ya zamani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 5, 2017

Thiery Henry: Ozil asingepata nafasi kwenye Arsenal yangu ya zamani


Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thiery Henry amemtuhumu Mesut Ozil kutokana na kucheza kivivu uwanjani.
Baada ya Arsenal kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Manchester City siku ya Jumapili, Henry alisema kuwa mchezaji huyo asingeweza kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal cha zamani kwa kiwango alichonacho baada ya mechi . “Anacheza vizuri sana, na mwaka jana kila mtu alikuwa akimsifu,” Henry ameiambia Sky Sports.
“Anapocheza ndani ya fulana ya Arsenal, wakati mwingine hachezi katika kiwango cha Arsenal. Namkubali sana na jinsi anavyocheza, lakini kama angekuwa kwenye timu yangu ya zamani, najua kulikuwa na wakali ambao wangemkabili na huenda ndicho anachohitaji,” ameongeza.
“Katika timu yangu ya zamani, kila mmoja alikuwa na fursa ya kuongea. Sylvain Wiltord aliongea. Edu kadhalika. Hata Nwankwo Kanu alikuwa na ya kusema. Jens Lehmann, alikuwa akiongea muda wote. Ni lazima ucheze kweli.”
Loading...

No comments: