MAX MALIPO YATANGAZA BODI MPYA, YAANIKA VIPAUMBELE VYA MIAKA 5 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 2, 2017

MAX MALIPO YATANGAZA BODI MPYA, YAANIKA VIPAUMBELE VYA MIAKA 5

Kampuni ya Maxcom Africa maarufu Max Malipo Jumanne hii imezindua bodi yake mpya ya Wakurugenzi pamoja na kueleza vipaumbele vya bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 5                    Mwenyekiti wa Bodi Prof. Samwel Wangwe akiwa na wajumbe wake.Uzinduzi huo ambao umefanyika makao makuu ya ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Millennium Tower jijini Dar es salaam ulihudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na wadu mbalimbali. Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, Mwenyekiti mteule wa Bodi Prof. Samwel Wangwe amesema watahakikisha kwa kipindi cha miaka mitano wanatimiza vipaumbele mbalimbali kikiwemo cha kuhakikisha watanzania wanapewa fursa ya kuimiliki kampuni hiyo kwa asilimia 25.   "Bodi hii itahakikisha kwamba kampuni ya Maxcom Africa-Max Malipo inakamilisha na kufanikisha mchakato uliowekwa kwa mujibu wa sharia wa kuuza asilimia 25% ya hisa zake za umiliki kwa watanzania, zoezi ambalo tunalianza mara Moja," alisema Prof. Samwel "Hili la hisa lina dhamira ya kuhakikisha kampuni hii inaendeshwa kwa kuzingatia matakwa na sheria za nchi yetu ya Tanzania ipasavyo.," [

Wajumbe wateule wa Bodi ya kampuni hii iliyozinduliwa Leo mbele ya wanahabari (kuanziakushotoni Ms. Lucy Kanza (Mjumbe), Mr. Ahmed Lusasi (Mjumbe), Eng. Juma Rajabu (Mjumbe),Prof. Samwel Wangwe (Mwenyekiti), Eng. George Mulamula – Mjumbe, Dr. DonalthUlomi (Mjumbe), Eng. Jameson Kasati (Mjumbe) 

Alisema bodi mpya itahakikisha kufikia 2022 itakua imefika kwenye nchi zaidi ya 10 barani Africa na kutoa ajira takribani 100,000 (LakiMoja) ambazo pia zitaiingizia serikali mapato makubwa kupitia kwenye kodi. Professa Wangwa amesema kampuni hiyo kufikia mwaka jana Desemba 2016 ilifanikiwa kuorodheshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye kundi la walipa kodi wakubwa Tanzania (Large Taxpayers). "Kampuni hii ilifanikiwa kulipa kodi takriban bilioni sita,"  alisema. Pia bodi hiyo imedhamiria kuhakikisha inasaidia serikali kufikia adhma yake ya kujitegemea, na kuwa nchi yenye mapato makubwa ya ndani, kutoka kwenye uchumi tegememezi na kuingia kwenye uchumi wa kisasa usiokuwa tegemezi. "Adhma hii tumejiwekea kwa kuhakikisha kwamba tuna wekeza katika Mifumo ya kielekroniki inayowezesha serikali kutambua vyanzo mbalimbali vya mapato.  Kudhibiti makusanyo pamoja na kuanisha njia za kisasa zaidi zinazoweza kuchangia kuifanya Tanzania yetu kujitegemea," alifafanua.   Bodi mpya ya  Kampuni ya Maxcom Africa – Maxmalipo
  1. MwenyekitiwaBodi : Samwel Wangwe
  2. Donald Olomi – Mjumbe
  3. George Mulamula – Mjumbe
  4. HashimLema – Mjumbe
  5. Juma Rajabu – Mjumbe
  6. Jameson Kasati – Mjumbe
  7. Ahmed Lussasi –Mjumbe
  8. Lucy Kanza – Mjumbe
         
Loading...

No comments: