Pogba apata pigo , afiwa na Baba yake mzazi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, May 14, 2017

Pogba apata pigo , afiwa na Baba yake mzaziBaba mzazi wa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, Fassou amefariki dunia jana usiku akiwa na umri wa miaka 79.

Fassou Antoine Pogba alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu kabla ya kukumbwa na mauti hayo familia ya Pogba imethibisha kutokea kifo hicho katiak hospitali ya Le Parisien.

Fassou mwenye asili ya Guinea alihamia Paris, Ufaransa miaka 30 iliyopita nchi ambayo Paul anaichezea katika mashindano ya kimataifa.

Watoto wake wengine ni mapacha Florentin na Mathias wenyewe wameamua kucheza nchi anayotokea baba yao Fassou.

Fassou alipiga picha akiwa jukwaani wakati wa fainali ya Euro 2016 zilizofanyika Ufaransa, akiwa na Florentin na Mathias  washangilia Paul akichezea Ufaransa dhidi ya  Uswisi.

Mwezi Machi, kiungo wa Manchester United, Paul alituma picha katika Instagram akisherekea sherehe ya baba yake kutimiza miaka 79.
Loading...

No comments: