SCOUT NJOMBE WAJITOLEA KUMCHANGIA DAMU MTOTO HASAN SHABAN NA KUNUSURU UHAI WAKE. May 18, 2017 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 23, 2017

SCOUT NJOMBE WAJITOLEA KUMCHANGIA DAMU MTOTO HASAN SHABAN NA KUNUSURU UHAI WAKE. May 18, 2017NJOMBE
|Na Sebastian Emmanuel jr
Vijana wa scout wa halmashauri ya wilaya ya njombe wamenusuru maisha ya mtoto mwenye umri wa miaka kumi kwa kujitolea kumchangia damu mtoto huyo aliekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuishiwa damu.

Mtoto huyo anaefahamika kwa jina la Hasan Shaban amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu ambapo mama mzazi wa mtoto huyo alichukua jukumu la kumpeleka hospitali ya kibena mkoani njombe ambapo alipewa huduma lakini bado tatizo la mtoto huyo liliendelea .

Licha ya baadhi ya jamii kuwa na dhana potofu ya kuwa endapo watatoa damu katika miili yao basi kuna matatizo ambayo wanaweza kuyapata lakini vijana hawa wamejitoa na kuamua kumsaidia mtoto huyo ambae kwa sasa amerejea katika hali yake ya awali tayari kuendelea na masomo yake.

Ni katika wodi aliyokuwa amelazwa mtoto hasan shaban ambapo nimefika kwa lengo la kumjulia hali mtoto huyu ambae kwa sasa unaisikia sauti yake ikiwa imara na tayari amerejea katika hali yake ya awali.

Gaspar Nziku na Ibrahim Msemwa ni miongoni mwa vijana wa scout ambao wamejitolea katika kumsaidia mtoto hasan kwa kumchangia damu ambapo vijana hawa wanasema kutoa damu hakuna madhara yeyote na wamefanya hivyo kwa kumsaidia mtoto huyo na kutimiza moja kati ya majukumu yao.

Mama wa mtoto hasani anaefahamika kwa jina la Tabita Yerunimsi likiriwike
 ameeleza jinsi ambavyo mtoto huyu aliivyoanza kusumbuliwa na tatizo hilo.

Kwa maelezo ya mama wa mtoto hasan imenilazimu kufahamu kuwa je, ni hatua zipi alifanya au ni ushauri upi waliompa madaktari mara tu baada ya kupewa taarifa hizo za kukatisha tamaa ?

Mtoto Hasani ana umri wa miaka kumi na ni mwanafunzi ambae ana ndoto na malengo aliyojiwekea kwaajili ya kumsaidia mama yake ambae ndio tegemeo kubwa kwa maisha yake ambae tatizo lake kubwa lilikuwa ni kupungukiwa damu na kiasi cha lita zipatazo mbili zilihitajika ili kunusuru uhai wake kama ambavyo mama yake anaendelea kueleza.

Bi Tabita ametumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa vijana wa scout ambao wamejitoa kumsaidia mtoto wake huku akieleza kuwa huenda wasinge kuwa vijana hawa basi mengine yangeongelewa kwa sasa.

Anita Ngole ni kamishna wa scout halmashauri ya njombe mjini ambae amewapongeza vijana wake huku akieleza siri ya vijana wake kuchukua jukumu la kufanya uzalendo waliouonesha kwa mtoto Hasan Shaban.

mbali na Msaada huu ambao vijana hawa wameamua kuutoa kwa mtoto hasan kuna baadhi ya vvijana na jamii kiujumla imejijengea dhana ya kuwa huenda kutoa damu kuna madhara kwaon je hili kamisha analisemeaje hasa katika jamii inayotuzunguka?

Pongezi kwa vijana hawa wa scout ambao wamejitoa na kunusuru maisha ya mtoto Hasan Shaban ambae kwa sasa afya yake imerejea na kuimarika zaidi.

Loading...

No comments: