Cosato Chumi aendelea kuwakumbuka wananchi wake. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, June 4, 2017

Cosato Chumi aendelea kuwakumbuka wananchi wake.

Mbunge wa mafinga mjini Mh. Cosato Chumi ameendelea kuwakumbuka waanchi wake wa jimbo hilo kwa kuendelea kuwatimizia ahadi zao, jana tarehe 3/6/2017 amewatembelea wananchi wa kata ya Isalavanu pamoja na kituo cha afya cha Ihongole kilichopo nje kidogo ya mji wa Mafinga. 
katika ziara yake hiyo akiwa shule ya sekondari ya Isalavanu amekabidhi  vitanda vya kulalia wanafunzi 35 ambavyo ni double dacker,  aidha mbunge huyo wa Mafinga mjini Cosato Chumi amekabidhi gari la kisasala kubebea wagonjwa kwa ajili ya kituo hicho cha Ihongole, pia chumi ametumia nafasi hiyo kumshukuru mh. Ummy Mwalimu waziri wa afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto kwa kumwezesha kupatikana kwa gari hiyo, amesema" asante sana kwa waziri wa afya wana Mafinga tunasema asante sana"
vitanda vikiwa tayari kukabidhiwa shuleni hapo
 Mh Cosato Chumi akimkabidhi vitanda diwani wa kata hiyo Challes makoga , ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mafinga


 Mh. Cosato Chumi akiongea na wananchi wakati wa kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha Ihongole.
 Mh Cosato Chumi akiwa ameshika utepe huku diwani wa kata hiyo Challes makoga , ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mafinga akiukata utepe huo kuashiria uzinduzi wa gari hilo la kubebea wagonjwa.
Loading...

No comments: