Tumikieni wananchi.........PHILIP MANGULA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, June 4, 2017

Tumikieni wananchi.........PHILIP MANGULA

NJOMBE                                                                                       
Ikiwa moja ya mikakati ya serikali ya awamu ya tano kwa watumishi wa umma ni utumishi uliotukuka, viongozi wateule ngazi ya mashina kupitia chama cha mapinduzi CCM kata ya Njombe mjini, wametakiwa kuwatumikia wananchi kikamilifu ili kuweza kuwatatulia changamoto wananchi hali ambayo itasaidia kukijenga chama hicho katika chaguzi zijazo.

Wito huo umetolewa na makamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania bara mh.PHILIP MANGULA wakati alipokutana na viongozi hao wa mashina katika ukumbi wa turbo, na kuwasisitiza viongozi na wanachama kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kujenga misingi imara ndani ya chama na Taifa.

Pamoja na wito huo, baadhi ya viongozi(BALOZI),wametumia fursa hiyo kumueleza kiongozi huyo wa chama taifa namna usaliti kwa wanachama na kuto kuwa na umoja kulivyo sababisha kupokwa kwa jimbo na chama pinzani huku wengine wakielezea kupuuzwa kwa ujenzi wa miundombinu hali ambayo huenda ikaendelea kuondoa imani kwa wananchi kuhusu serikali yao.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe EDWIRN MWANZINGA kwa upande wake ameahidi kushirikiana na halmashauri pamoja na wananchi kuendelea kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuwataka viongozi hao kuwa waogo katika maswala ya uongozi.

Katika hatua nyingine zoezi hilo la kukutana viongozi wa mashina limeambata na kuwapokea na kuwakabidhi kadi wanachama wapya ishirini katika kata ya mji mwema, pamoja na ugawaji wa bendera na kofia za  chama hicho kwa viongozi wateule. 

makamu mwenyekiti wa ccm Bara mzee Philip Mangula akitafakari jambo wakati wa mkutano huo


Loading...

No comments: