Kiungo mpya wa Yanga SC atua leo mazoezini - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 31, 2017

Kiungo mpya wa Yanga SC atua leo mazoezini


Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mbeya City, Raphael Daud kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji, Raphael Daud 
Daud anatarajiwa kujiunga leo katika mazoezi ya klabu hiyo ambayo imeweka kambi yake mjini Morogoro.
Yanga imemsajili Daud kwa ajili ya kuimarisha eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na mapungufu makubwa hasa baada ya kumkosa, Haruna Niyonzima kwaajili ya  msimu ujao.
Loading...

No comments: