Barakah Da Prince ananiita Baba – Dully Sykes - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 18, 2017

Barakah Da Prince ananiita Baba – Dully Sykes

Legendary wa Bongo Flava, Prince Dully Sykes, amedai kuwa msanii wa muziki anayemiliki lebo ya Bana, Barakah The Prince anamuita baba katika muziki.
Kupitia kupindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Dully amebainisha hayo baada ya kusema kuwa Barakah The Prince anamuita baba na Young Dee anamuita babu katika muziki, kauli hiyo ya Dully imekuja baada ya kueleza kuwa yeye ndiye aliyetoa jina kwa msanii huyo.
“Nilimpa jina la Da Prince jina ambalo limeishia na mimi, Baraka ananiita Baba na Young Dee ananiita Babu kwa kuwa aliletwa na mwanangu Mr. Blue,” amesema Dully.
Dully ni moja ya watu walipo katika mainstream ya mzuiki wa Bongo Flava kwa muda mrefu na amekuwa akifanya vizuri kwa wakati wote, pia amekuwa na mchango kwa baadhi ya wasnii waliopo katika muziki, Dully anaendelea kuheshimika kutoka na kutopenda kutengeneza kiki kitu ambacho hata yeye amekuwa akikataa na kusema yeye ni mtu mzima hawezi kufanya hivyo.
BONGO 5
Loading...

No comments: