Fid Q atamani albamu yake kutumika mashuleni - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 18, 2017

Fid Q atamani albamu yake kutumika mashuleni

Msanii wa hip hop Bongo, Fid Q ameweka wazi ubora wa albamu yake ya tatu ‘Kitaa Olojia’ ambayo ipo mbioni kutoka.
Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya ‘Fresh’, ameiambia Clouds 360 ya Clouds Tv kuwa albamu hiyo itakuwa na mafunzo ya kiwango cha juu kabisa kiasi kwamba itafaa kufundishia mashuleni.
Katika hatua nyingine Fid Q ameeleza kuwa ana ngoma nyingi sana hadi ukifika wakati wa kutoa ngoma anashindwa kuchagua atoe ipi.
“Mashabiki zangu hawaangalii beat za ngoma zangu bali wanasikiliza naimba nini na mashairi ya aina gani kwa wakati huo” amesema Fid Q.
Loading...

No comments: