KAMATI YA UJENZI WA ZAHANATI NJOMBE YAJIUZURU. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, August 2, 2017

KAMATI YA UJENZI WA ZAHANATI NJOMBE YAJIUZURU.


 wananchi walio jitokeza katika mkutano huo wa hadhara.

mwenyekiti wa kamati hiyo ya ujenzi akiongea jambo mbele ya wananchi walio jitokeza katika mkutano huo wa hadhara.

NJOMBE, Na Sebastian Emmanuel jr.
                                                                   
Kamati ya ujenzi wa zahanati ya mtaa wa matalawe na Buguruni Halmashauri ya mji wa Njombe imejiuzulu kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika taarifa iliyosomwa na mkaguzi mkuu wa fedha CAG halmashauri ya mji wa Njombe.

Aidha kutokana na maombi yaliyotolewa na wananchi wa mitaa hiyo katika mkutano uliofanyika katika eneo la zahanati hiyo imeitaka kamati kujiuzulu na kutolea ufafanuzi juu ya mapungufu hayo huku wananchi wengine wakienda mbali nakuwataka wale wote watakaobainika kusababisha mapungufu hayo hususani matumizi mabaya ya fedha kufikishwa mahakamati.
Akitoa taarifa ya ukaguzi wa zahanati hiyo mkaguzi mkuu wa halmashauri ya mji ndug.JAPHET MAJIGE ametaja miongoni mwa mapungufu aliyo yabaini katika mradiwa ujenzi wa zahanati hiyo ni mapungufu katika stakabadhi ya kukusanyia mapato hali anayopelekea kupungua kwa mapato na kushindwa kukamilika ujenzi kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo  kumesababisha miongoni mwa wananchi akiwemo EVARIST LUPENZA kuiomba kamti hiyo kutumia busara ya kujiuzuru ili kuweza kupisha watu wengine watakao weza kusimamia ujenzi huo.
Kauli ya wananchi hao katika mkutano imemfanya mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ndugu ZAWADI MTWEVE kwa niaba ya kamati kuomba kuachia nafasi ili kupisha kamati nyingine itakayo weza kukamilisha ujenzi.
Aidha wazo la ujenzi wa zahanati  hiyo lilianza tangu mwaka 2010 na kuanza ujenzi ambapo kutokana na ramani ya jengo  ilikadiliwa milioni arobaini na saba mia tano tisini na sita elfu ambapo kufikia sasa kiwango cha fedha kilichotumika ni milioni hamsini na nne mia tisi ishirini na mbili, lakini bado zahanati hiyo haijakamilika, aidha mara baada ya kujiuzuru kwa kamati hiyo wananchi wameadhimia kuunda kamati  mpya jumapili ya tarehe 6 mwezi wa 8 mwaka huu.
Loading...

No comments: