MAONESHO YA NANENANE YA NYANDA ZA JUU YAZINDULIWA KATIKA VIWANJA VYA MWAKANGALAE MBEYA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, August 1, 2017

MAONESHO YA NANENANE YA NYANDA ZA JUU YAZINDULIWA KATIKA VIWANJA VYA MWAKANGALAE MBEYA.

 washiriki wa maonesho hayo wakitolea ufafanuzi juu ya bidhaa wanazo zitengeneza kwa wageni walio fika katika maonesho hayo ya wakulima maalufu kama maonesho ya Nane Nane.


 Mgeni Rasmi  na mkuu wa Mkoa wa Songwe akisikiliza kwa makini maelezo ya washiriki wa maonesho ya wakulima katika viwanja vya nane nane mkoani Mbeya maalumu kama Viwanja vya John Mwakangale.

 pia kulikuwepo na burudani za Ngoma za asili katika maonesho hayo.
 mgeni rasmi akitafajari jambo kabla ya kualikwa kwenda kuhutubia maelfu ya wananchi wali jitokeza katika viwanja vya John Mwakangale kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nane Nane.
 mgeni rasmi akihutubia maelfu ya wananchi wali jitokeza katika viwanja vya John Mwakangale kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nane Nane.
baadhi ya wananchi walio toka katika maeneo mbali mbali, walikuwa wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio yaliyo kuwa yakiendelea katika viwanja hivyo

Na sebastian Emmanuel jr, Mbeya
Maonesho ya  wakulima (Nane nane) kitaifa yatazinduliwa tarehe 3.8.2017 katika mkoa wa Lindi, huku kwa upande wa nyanda za juu kusini ikihusisha mikoa sita (6)  ya Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Songwe, na Mwenyeji Mbeya.
Maonesho hayo ambayo yamepokelewa kwa hamu kubwa na wakazi wa mikoa hii ikiwa ni fursa kwao kushuhudia shughuli mbalimbali maonesho ya kilimo, ufugani pamoja na ujasilia mali. pamoja na hayomaonesho hayo yamekwenda pamoja na uhimizwaji wa uwepo wa sera ya Serikali ya Tanzania ya viwanda inayo anza na wakulima.
Maonesho hayo yamezinduliwa na Waziri wa viwanda na Biashara (mb) Charles Mwijage aliye wakilishwa na Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Msataafu Chiku Galawa, Mkuu huyo wa mkoa amesema anategemea kuona Ushiriki wa kila Halmashauri katika maonesho hayo yanayo fanyika katika viwanja maalufu vya John Mwakangale vilivyopo katikati ya jiji la mbeya ambapo mkuu wa mkoa wa Mbeya aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Aidha Galawa amesema kuwa serikali inaamini kuwa kipindi cha mda mfupi tuu baadhi ya kelo za wakulima zitamalizika kabisa kwa kuwa tayari wameweka utaratibu unaowapa nafuu wakulima kuondokana na kelo za kimasoko na kimfumo ama mfumo mbovu uliokuwepo kipindi cha nyuma.
Maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa katikati Viwanja hivyo siku ya Tarehe 8/8/2017 na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Samia Suruhu hassani.
 
Loading...

No comments: